Rais mpya wa FIFA yuko Sudan Kusini

Image caption Rais mpya wa FIFA yuko Sudan Kusini

Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino amefungua afisi ya shirikisho la kandanda la Sudan Kusini katika safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu achaguliwe rais wa shirikisho hilo la soka duniani mwezi uliopita.

Infantino alilakiwa kwa shangwe na vigelegele na wenyeji wake.

Aidha Infantino alitumia ziara hiyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Image caption Aidha Infantino alitumia ziara hiyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Mkuu huyo wa fifa sasa ametimiza miaka 46.

Rais huyo wa FIFA ameratibiwa kufanya mkutano na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir mjini Juba kabla ya kushuhudia mechi ya kuwania kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika kati ya Sudan Kusini na Benin.

Image caption Ukienda Roma jifunze kirumi

Picha kutoka Juba zinamuonesha Infantino akisherehekea kwa keki na nyimbo siku yake ya kuzaliwa.

Kama ilivyoada alivishwa mavazi ya kitamaduni na wenyeji wake.