Mc Hale Kuchuana na Serena

Haki miliki ya picha .
Image caption Serena Williams kukipga na MC Hale

Mcheza Tenesi Christina Mc Hale raia wa Marekani amemshinda Misaki Doi wa japani katika michuano ya wazi ya Miami.

Mchale alishinda kwa jumla ya seti 6-2 kisha akapoteza kwa 4-6 na kumaliza na ushindi wa seti 7-5,katika raundi ya mwisho.

Kwa ushindi huo nyota huyu wa tenesi atachuana na nyota namba moja wa kwa ubora wa mchezo huo Serena Williams, katika raundi inayofuata.

Katika raundi nyingine Mfaransa Alize Cornet alimshinda Galina Voskoboeva wa Kazakhstan hivyo mfaransa huyu atachuana na Agnieszka Radwanska, huku Julia Goerges wa Ujerumani akimshinda Nao Hibino wa Japani na hivyo atacheza na Samantha Stosur raia wa Austalia katika mchezo unaofuata..