Matokeo ya mechi za kirafiki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu ya Hispania
Usiku wa kuamkia leo kumechezwa michezo ya kirafiki ya kimataifa ikiwa ni michezo ya kujiandaa na michuano ya kombe la ulaya.

Mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2010 Hispania walitosha nguvu na itali kwa kufunga bao 1-1,Uturuki wakapata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Swedeni.

Malta wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wameambulia sare ya 0-0 na Moldova, Norway na Estonia nao wakashindwa kutambiana baada ya kwenda sare ya bila bila.

Matokeo mengine

Ugiriki 2-1 Montenegro 1

Denmark 2 -1Iceland 1

Ukraine 1-0 Cyprus 0

Jamuhuri ya Czech 0-1 Scotland

wales 1-1 Ireland ya kaskazini