Mourinho na mikakati kuiboresha Man utd.

Haki miliki ya picha Getty

Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atachukua nafasi ya Louis van Gaal.

Kwa mujibu wa jarida la Don Balonna Mourinho anataka kusajili nyota watatu.

Kocha huyo ameshaanza mipango ya usajili kwa kuweka wachezaji kadhaa nyota katika orodha yake akiwemo mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata.

Mourinho ameshawahi kufanya kazi na Higuain wakati akiwa Madrid na United wameonyesha kuwa tayari ingawa watalazimika kulipa kitita cha paundi milioni 58 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina.

United pia watakabiliwa na upinzani kwa Morata ingawa Madrid wako tayari kumnunua tena kama mkataba unavyotaka ili waje kumuuza kwa kiwango cha juu wakati Rodriguez yeye anatarajiwa kuondoka kiangazi kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.