Murray na Watson wasonga mbele.

Haki miliki ya picha AFP

Wachezaji Andy Murray na Heather Watson wote wamesonga mbele katika michuano ya wazi ya Miami.

Murray akicheza katika mazingira magumu ya hali ya hewa amemshinda Denis Istomin kwa seti 6-3 7-5.

Kwa upande wake Watson amemshinda Yanina Wick-mayer seti 3-6, 7-5, 6-3 katika mchezo uliodumu masaa mawili na nusu.

Kwa upande mwingi Briton Aljaz alilazimika kutoka nje ya mchezo kutokana na jeraha la mkono, huku Jamie Murray akipoteza mchezo wake.