England yalazwa na Uholanzi, Ureno watamba

Haki miliki ya picha Reuters

Katika Mechi za kirafiki za kimataifa zilizochezwa jana Ureno wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ubelgiji.

England imeonja joto ya jiwe kwa kuchapwa na Uholanzi magoli 2-1, Ufaransa imetakata dhidi ya Urusi kwa ushindi wa magoli 4-2, Scotland imeifunga Denmrk 1-0.

Estonia imepigwa na Serbia kwa kufungwa bao 1-0, Georgia imetoka sare na Kazakhstan ya bao 1-1, Macedonia imekubali kichapo kutoka kwa Bulgaria ca bao 1-0.

Greece imefungwa na Iceland bao 3-2, Norway imeshinda dhidi ya Finland bao 2-0, Montenegro na Belarus nguvu sawa 0-0, Georgia na Kazakhstan zimetoka sare pacha ya bao 1-1.

Hayo ni matokeo ya mechi za kirafiki za kimataifa.