Konta afungwa na Azarenka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Victoria Azarenka

Johanna Konta amefungwa na Victoria Azarenka katika mchezo wa robo fainali michuano ya wazi ya Mayami.

Konta ambaye alifikia mwisho mara ya nane ya mashindano hayo, alifungwa seti 6-4, 6-2 na mpinzani wake Kibelarusi ndani ya dakika 90.

Azarenka mwenye miaka 26, amekuwa akijifua zaidi na hii ni baada ya kumfunga Serena Williams katika michuano ya India Wells mapema mwezi huu.

Konta awali alishindwa kubadilisha matokeo zaidi akiwa na pointi tano hadi mapumziko.