El-Clasico: Barcelona kumenyana na R Madrid

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Barcelona dhidi ya Real Madrid

Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa yeye na wachezaji wake hawana shinikizo yoyote kabla ya mechi ya El Clasico kati ya Real Madrid na Barcelona katika uwanja wa Nou Camp.

Viongozi wa ligi Barcelona wako pointi 10 mbele ya wapinzani wao na wanakaribia kushinda taji la tatu katika misimu minne.

Haki miliki ya picha
Image caption Zidane

Real Madrid ambayo ilitawazwa mabingwa wa La Liga mnamo mwaka 2012 iko katika nafasi ya tatu huku ikiwa kuna mechi nane zilizosalia.

''Nimetulia,Hii ni soka na nitajifurahisha,''alisema Zidane siku ya Ijumaa.