MOJA KWA MOJA: Arsenal dhidi ya Watford

Ligi Kuu ya Uingereza inarejea wikendi hii baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa Jumamosi kukiwa kumeratibiwa mechi kati ya Aston Villa na Chelsea ,Arsenal dhidi ya Watford miongoni mwa mechi nyengine.

18.35pm:Watford wanafukuza vivuli vya wachezaji wa watford hapa ikiwa ni dakika ya 85

18.31pm:Watford inaendelea kuisukuma nyuma Arsenal lakini bahati haijakuwa yao

18.30pm:Alexi Iwobi atoka kwa upande wa Arsenal na mahala pake panachukuliwa na Theo Walcot

18.28pm:Goaal la Nahodha wa kikosi cha Watford Deaney ageuka na kupiga tobwe moja la maudhi lakini kipa wa Arsenadl david Ospina aupangua kabla ya kuokoa kona.

Image caption Iwobi

18.26pm:Wellbeck atoka na Giroud aingia kwa upande wa Arsenal

18.22pm:Arsenal inaendelea kuongoza bao tatu kwa bila dhidi ya Watford ikiwa ni dakika 22 ya kipindi cha pili

Image caption Sanchez na Iwobi hapa

18.11pm:Arsenal inatawala mchezo hapa.Utadhani sio timu waliocheza nayo katika kombe la FA.

18.05pm:Goooooooooal Bellerin aipatia Arsenal bao la tatu hapa

18.05pm:Kipindi cha pili cha mechi kati ya Arsenal dhidi ya watford kinaanza

18.00pm:Matokeo ya #EPL baada ya kipindi cha kwanza

  • Aston Villa 0- 4Chelsea
  • Arsenal 3-0Watford
  • Bournemouth 0 -3 Man City
  • Norwich 1- 0 Newcastle
  • Stoke 1- 0Swansea
  • Sunderland 0- 0West Brom
  • West Ham 2-1 Crystal Palace

17.50pm:Kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Arsenal dhidi ya Watford kinakamilika ikiwa

Arsenal 2-0 Watford

17.30pm:Goooooooooal Arsenal yapata bao la pili hapa kupitia Iwobi

Image caption Bellerin

17.20pm:Kumbuka watford ndio timu iliobandua arsenal katika kombe la FA majuma mawili,Mechi iliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Emirates.

17.18pm:Kona inapigwa lakini walinzi wa watford wanautoa mipra katika eneo la hatari na baadaye mpiura unatoka kuelekezwa lango la Arsenal

Image caption Coquelin

17.16pm:Sancheeez apiga mkwaju wa adhabu lakini kipa aupangua hapa ,Kona

17.15pm:Wachezaji wa Arsenal akiwemo Iwobi na El Neny wanaonekana kutulia sana

Image caption Iwobi

17.10pm:Iwobi apiga kombora zuri lakini mlinda lango wa Watford anaupangua mpira

Image caption Alexi Sanchez akimpongeza Iwobi

17.07pm:Gooooooooooal Arsenal inajiweka kifua mbele hapa kupitia Alexi Sanchez baada pasi nzuri kutoka kwa Iwobi.

Image caption Ozil akitamba na mpira

17.06pm:Arsenal inaanza mechi kwa kasi hapa ikiwa hakuna timu ilioona lango la mwenziwe.

17.00pm:Mechi inaanza

Image caption Kikosi cha Arsenal
Image caption Kikosi cha Watford
Arsenal vs Watford.