Djokovic atwaa taji la wazi Miami

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Novak Djokovic

Nyota namba moja kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani kwa wanaume Novack Djokovic ameendelea kutamba katika mchezo huo.

Djokovic ametwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Miami kwa kumshinda mpinzani wake Kei Nishikori, kwa kumchapa kwa jumla ya seti mbili kwa 6-3 6-3.

Ushindi huo unampa nyota huyu wa tenesi taji la 63 toka alivyoanza kucheza mchezo huu katika ngazi ya ushindani.

Mchezaji huyu ameingiza kaisi cha $1,028,300 baada ya mchezo huo na kuwa anaongoza kwa wacheza tenesi wanaoingiza pesa nyingi na akiwa amefikisha kiasi cha $100 million, katika muda aliocheza mchezo huo.