Luke Shaw arejea mazoezini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Luke Shaw

Beki wa kushoto wa Man United Luke Shaw ameanza kufanya mazoezi na wenzake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi saba.

Mlinzi huyu alivunjika mfupa wa mguu mara mbili katika mchezo wa klabu bingwa ulaya mwezi September walipokua wakicheza na Pvs.

Shaw mwenye umri wa miaka 20 alichezewa rafu mbaya na mlinzi wa Psv, Hector Moreno iliyompelekea kukaa nje ya dimba kwa miezi saba.

Kiungo wa timu ya Man United Juan Mata aliweka picha ya beki huyo akifanya mazoezi na wenzake katika ukurasa wake wa mtandano wa Instagram.

Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Taifa ya England, Shaw bado ananafasi ya kuitwa kwenye timu ya taifa itakayoshiriki michuano ya Euro 2016.