Barcelona, Bayern zashinda

Haki miliki ya picha AP
Image caption Furaha ya mwanzo mwema

Timu za Barcelona na Bayern Munich zimeanza vizuri michezo yao ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya.

Barcelona, wakicheza katika uwanja wao wa Camp Nou, wamechomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid, mshambuliaji Luis Suarez akifunga mabao yote mawili.

Na bao la Atletico Madrid likifungwa na Fernando Torres ambae pia alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano.

Nao Bayern Munich wakiwa wenyeji wa Benfica wameshinda kwa bao 1-0 kwa bao lilowekwa kambani na kiungo Arturo Vidal.