Azam yavutwa shati,Majimaji yapeta

Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea tena leo hii kwa michezo miwili kuchezwa

Azam Fc wakicheza katika uwanja wao wa Azam Complex,walivutwa shati na Ndanda Fc kwa kukubali sare ya mabao 2-2.

Mabao ya Azam yalifungwa na Ramadhani Singano na Didier Kavumbagu huku mabao ya Ndanda yakifungwa na Atupele Green kwa mkwaju wa penalti nae Hemed Msumi aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili.

Maji maji nao wakachomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, baada ya mchezo huo Coastal Union wanaendelea kuburuza mkia wakiwa na alama 19 wakiwa wamecheza michezo 26