Kashfa ya Panama yatinga FIFA

Image caption Juan Pedro Damiani

Kiongozi mkubwa katika shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, amejiuzulu wadhifa katika tume ya maadili baada ya jina lake kuonekana katika kashfa ya matumizi mabaya ya fedha ya PANAMA.

Juan Pedro Damiani,wakili kutoka Uruguay,ndiye mwanzilishi wa kamati hiyo ya maadili.kuvuja kwa nyaraka hizo kunaashiria kwamba kampuni yake ilifanya kazi kwa ajili ya makampuni saba ambazo zina uhusiano na Eugenio Figueredo, makamu wa raisi wa zamani wa shirikisho hilo ambaye anakabiliwa na kashfa ya rushwa nchini Marekani.

Lakini kumbukumbu hazioneshi uwepo wa shughuli yoyote isyohalali.kamati ya maadili ya FIFA inafanya uchunguzi endapo kanuni za maadili zimevunjwa. Juan Pedro Damiani amekana shutuma zinazomkabili.