Don Bosco wanyakua ubingwa wa vikapu Dar

Image caption Timu ya mpira wa Kikapu,Savio

Timu ya Mpira wa Kikapu ya Savio kutoka Don Bosco Youth Center Upanga wamenyakua ubingwa katika jiji la Dar es Salaam kwa kuwafunga wapinzani wao Vijana City Bulls kwa vikapu 66-59.

Ligi hiyo iliyoanza mwaka jana mwezi wa 10 imekamilika kwa kuziruhusu timu hizi mbili za juu kushiriki katika Ligi Kuu ya Taifa yaani NBL ambayo itakamilika kwa kuipata Club bingwa ya Kikapu nchini Tanzania.K

ocha wa savio Isihaka Masoud ndiye amechukua tuzo ya kocha bora wa mwaka wa michuano hiyo.