Wambach akiri kutumia mihadarati

Image caption Abby Wambach

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Marekani Abby Wambach amekiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine pamoja na uvutaji wa bangi.

Wambach mshindi wa kombe la dunia la wanawake na michuano ya Olimpic mara mbili alikamatwa siku ya jumamosi kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Mchezaji huyu wa zamani alifikishwa mahakamani siku ya jumanne katika mahakama Multnomah County Circuit Court.

Katika nyaraka za mahakama, zimeandikwa kuwa alianza kutumika bangi akiwa na umri 24 na matumizi yake ya mwisho ilikuwa saa 25 zilizopita.