Matokeo ya mechi za Europa Ligi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jezi namba 17 Divock Origi

Michezo minne ya robo fainali ya michuano ya Europa ligi imechezwa katika viwanja vinne tofauti.

Liverpool wakiwa ugenini nchini Ujerumani walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Borrusia Dortmund, Divock Origi aliwafungia Liverpool bao la kuongoza kabla ya beki wa Dortmund Mats Hummels kusawazisha.

Sevilla wakawachapa ndugu zao wa Athletic Bilbao kwa mabao 2-1mabao ya ushindi ya Sevilla yakifungwa na Timothee Kolodziejczak na Vicente Iborra, huku bao la kufutia machozi la Bilbao likifungwa na Aduriz Zubeldia.

Sporting Braga wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk walikubali kulala kwa kichapo cha mabao 2-1,wachezaji Yaloslav Rakitskiy na Facundo Ferreyra wakifunga mabao ya ushindi, huku Naval Costa Eduardo kwa Braga.

Villarreal wakicheza katika dimba la El Madrigal wlichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sparta Prague, Cedric Bakambu akifunga mabao yote mawili kwa upande Villareal huku Jakub Brabec akifunga bao pekee la Sparta.