LeRoy: kazi ngumu Togo

Haki miliki ya picha getty
Image caption Kocha Claude kazini,Togo.

Kocha mpya wa kikosi cha timu ya taifa ya Togo Claude LeRoy amesema anatambua ugumu ataokutana nao katika kuimarisha soka la nchi hiyo.

LeRoy, mwenye umri wa miaka 68 amechukua nafasi ya Tom Saintfiet,aliyekua akihangaika kuisadia Togo kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Africa 2017.

" Najua itakua ngumu, tuna nafasi ndogo sana ya kufuzu kwa michuano ijayo ya Africa, na Togo wanatakiwa kutengeneza soka la ndani, alisema kocha huyo akizungumza na BBC.

Kocha huyu amefundisha soka barani Afrika Kuanzia Mwaka 1986 akiwa kocha wa Cameroon na kabla ya kuwa kocha wa Togo alikua akikinoa kikosi cha Congo.