Riek Machar kurejea Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Getty

Kiongozi wa waasi Sudan Kusini Riek Machar amesema kwamba atarejea kutoka uhamishoni siku kumi zijazo za mwezi huu.

Riek aliikimbia nchi hiyo mara baada tu ya kuzuka kwa vita vya vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2013, na amekuwa akiishi uhamishoni nchini Ethiopia.

Uamuzi wake huo wa kurejea nyumbani ni uamuzi muhimu kutokana awali kuundwa kwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.uwepo wa serikali hiyo ni chini ya masharti ya mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi March mwaka wa jana, na Machar anaelezwa kuwa atakuwa makamu wa kwanza wa rais.

Tangu vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka nchini Sudan Kusini,maelfu ya raia waliuawa na wengine zaidi ya milioni mbili wameyakimbia makazi yao.