Leicester City yaendeleza ubabe EPL

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Leicester City imefikisha alama 72 katika msimamo wa Epl

Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena jumapili kwa michezo mitatu ,Sunderland wakicheza nyumbani dhidi ya vinara wa ligi Leicester city, waliambulia kipigo cha mabao 2-0, na kuwafanya leicester city kufikisha alama 72 katika Msimamo.

Liverpool waliibamiza stoke city kwa kichapo cha mabao 4-1 yaliyofungwa na wachezaji Alberto Moreno, Daniel Sturridge na Divock Origi (mabao mawili) huku bao pekee la kufutia machozi la Stoke City likifungwa na Bojan Krikic.

Na Mechi ya tatu ya mwisho kati ya Tottenham na Manchester united mchezo ulimalizika kwa United kuchabangwa mabao 3-0.

Dakika ya 70 mchezaji Dele Alli alianza kuiptia goli bao la kwanza Tottenham .

Tottenham iliandika bao la pili kupitia kwa Toby Alder-weireld, huku bao la tatu likipachikwa na Erick Lamela dakika ya 76.