China kujenga viwanja 60,000 katika miaka 6

Haki miliki ya picha BBC CHINESE
Image caption Viwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya.

China inapania kujenga viwanja 60,000 vya Kandanda katika kipindi cha miaka 6 ijayo.

Image caption Uwanja wa taifa wa Beijing

Hayo ni baadhi ya mapendekezo katika ruwaza ya kandanda ya China ya 2050 ya kuifanya nchi hiyo iwe kati ya mataifa makuu duniani katika kandanda.

Ripoti moja ya serikali imeelezea mipango ya kuimarisha idadi ya wachezaji na watoto wanaosakata dimba kutimia watoto milioni 50.

Haki miliki ya picha Xinhua News Agency
Image caption China inalenga kuwa na wachezaji milioni 50 katika miaka 30 ijayo

Viwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya.

Kulingana na ruwaza hiyo China itakuwa na vilabu vyenye hadhi ya kimataifa kufikia mwaka wa 2050.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia

Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia la kandanda na hata kushinda kombe la dunia.

Aidha rais Jinping pia anaitaka kombe la dunia la kandanda liandaliwa nchini mwake.