Tanzania: Simba yachinjwa kombe la Shirikisho

Image caption Kikosi cha Simba kimeondolewa Kombe la Shirikisho

Hatua ya Robo fainali ya mwisho ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania (Federation Cup) imepigwa kati ya Coastal Union dhidi ya Simba katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na huku coastal Union

ikifanikiwa kuitoa Simba katika michuano hiyo kwa ushindi wa Bao 2-1.

Magoli ya coastal yamefungwa na Mchezaji wa Cameroon Youssouf Sabo,huku goli la Simba likifungwa na Mganda Hamisi Kiiza.

Coastal sasa inajumuika na Yanga, Azam FC na Mwadui kwenye Droo ya kupanga Mechi za hatua ya Nusu Fainali itakayofanyika Jumanne .

Mshindi wa Michuano hili ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).