Monte Carlo:Murray kumvaa Benoit Paire

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Andy Murray asonga mbele robo fainali ya Monte Carlo Masters

Mchezaji wa tenisi namba mbili duniani Andy Murray amefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Monte Carlo Masters baada ya kumfunga Benoit Paire.

Mwingereza huyo ameshinda kwa seti 6-2, 7-5 7-5 katika muda wa saa mbili na dakika 33 dhidi ya Mfaransa huyo.

Murray mwenye miaka 28, sasa atakabiliana raia wa Canada Milos Raonic na Roger Federer huenda akachuana na Rafael Nadal au Stan Warinka.