City wapewa Real Madrid ligi ya mabingwa

Pep Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pep Guardiola atakuwa meneja wa Manchester City msimu ujao

Klabu ya Manchester City ya Uingereza imeepuka kukutana na meneja wake wa msimu ujao Pep Guardiola kwenye nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Miamba hao wa Uingereza wamepwa Real Madrid ya Uhispania.

Bayern Munich wa Ujerumani, ambao kwa sasa wamo chini ya Pep Guardiola watakutana na Atl├ętico Madrid ya Uhispania.

Safari ya kuelekea Milan

Droo ya nusufainali Ligi ya Mabingwa Uefa 2016

Manchester City (Uingereza) v Real Madrid (Uhispania)

Atletico Madrid (Uhispania) v Bayern Munich (Ujerumani)

Allsports

Mpangilio huo natoa nafasi ya kuwepo debi ya Madrid fainali iwapo Atletico na Real zitafika fainali au hata kukutanisha Pep Guardiola na klabu yake ya msimu ujao fainali iwapo City na Bayern watafuzu.

Man City watakuwa nyumbani dhidi ya Real Madrid Jumanne 26 Aprili, na ugenini Bernabeu Jumatano 4 Mei.

Atletico Madrid watakutana na Bayern Munich nyumbani Jumatano 27 Aprili na mechi ya marudiano iwe Ujerumani Jumanne tarehe 3 Mei.

Katika Europa League, klabu ya Liverpool ya Uingereza imekabidhiwa Villarreal ya Uhispania katika hatua ya nusu fainali.

Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine nao watakutana na mabingwa watetezi Sevilla.

  • Liverpool v Villarreal
  • Shakhtar Donetsk v Sevilla

Liverpool walifika nusufainali kwa kulaza Borussia Dortmund Alhamisi kwenye mechi ya kusisimua wakitoka nyuma 2-0 wakati wa mapumziko na kushinda 4-3 uwanjani Anfield.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa mkufunzi wa Borussia Dortmund

Walifanikisha ushindi wa jumla wa 5-4.

Sevilla, ambao wanapigania kushinda kikombe kwa mara ya tatu mtawalia, walitinga nusufainali kwa kuwashinda Athletic Bilbao kupitia mikwaju ya penalti.