Leicester, Arsenal zashindwa kutamba

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Andy Carroll akiwajibika

Vinara wa ligi kuu ya England walishindwa kuutumia vyema uwanja wao nyumbani wa King Power kwa kukubali sare ya mabao 2-2 na West Ham .

Jamie Vardy, aliipa Timu yake uongozi kwa Bao 1 katika dakika ya 18, mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll,akasawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati kabla ya Aaron Cresswell kuongeza bao la pili kwa upande wa Wagonga nyundo.

Katika dakika ya lala salama Jose Leonardo Ulloa akaisawazishia Leicester kwa goli la mkwaju wa penati. Nao Arsenal wakicheza katika dimba la Emirates waliambulia sare ya bao 1-1 na Crystal Palace, Alexis Sanchez alianza kuifungia timu yake kabla ya Yannick Bolasie, kusawazisha bao hilo.

Liverpool wakachomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fc Bournmouth kwa mabao ya Roberto Frimino na Dan Sturridge huku bao pekee la Bournmouth likifungwa na Joshua King.