Toto yawavuta shati Simba

Toto Africans, wamewazuia wekundu wa Msimbazi Simba Sport klabu kurejea kileleni mwa ligi kuu Tanzania.

Baada ya kuwachapa kwa bao 1-0 katika mchezo ulichezwa kwenye uwanjwa wa taifa Jijini ya Tanzania, Dar es Salaam

Bao lililopeleka simanzi Msimbazi lilifungwa Dakika ya 20 ya mchezo na mchezaji Waziri Shentembo kwa Shuti kali lililopigwa toka umbali wa la Mita 25.

Katika mchezo huu Kocha wa Simba Jackson Mayanja, na beki mahiri wa kikosi hicho Hassan Kessy walilabwa kadi nyekundu.

Matokeo haya yamewaacha Simba Nafasi ya Pili wakiwa na pointi 57 kwa michezo 25 huku Yanga wakiwa kileleni wakiwa na pointi 59 kwa michezo 24. Huku Azam Fc wapo nafasi ya 3 wakiwa na pointi 55 kwa mechi 24.