Messi alivyofunga mabao yake 500

Messi Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mabao mengi ya Messi ameyafunga kwa mguu wa kushoto

Mshambuliaji matata kutoka Argentina Lionel Messi hatimaye alifunga bao lake la 500 katika maisha yake ya uchezaji Jumapili.

Alifunga bao hilo dakika ya 63.

Bao lake hata hivyo halikutosha kuzuia Barcelona wasipokezwe kichapo chao cha tatu mtawalia katika La Liga, mara ya kwanza tangu 2003.

Barca walichapwa 2-1 na Valencia.

Ni karibu miaka 11 tangu Messi afunge bao lake la kwanza la ushindani akiwa na umri wa miaka 17.

Bao hilo lilikuwa dhidi ya klabu ya Albacete mwezi Mei 2005.

"Idadi hiyo ya mabao ni kama inatoka sayari nyingine,” mkufunzi wa Barca Luis Enrique alisema kuhusu ufanisi huo.

Hapa, tunaangalia jinsi mshambuliaji huyo wa Argentina alivyofungia taifa na klabu mabao hayo: