Spurs washinda na kutishia Leicester

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Harry Kane

Klabu ya soka ya Tottenham wakicheza ugenini katika dimba la Brittania wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.

Kwa ushindi huo Spurs wanafikisha alama 68 wakiwa wamecheza michezo 34, hivyo kupunguza pengo dhidi ya vinara Leicester City kufikia alama 5,huku wakiwa wanalingana michezo waliyocheza.

Mshambuliaji mahiri wa kikosi cha Spurs Harry Kane alianza kuzifumania nyavu katika dakika ya tisa ya mchezo, kisha kiungo Delle Ali akaongeza bao la pili katika dakika ya 67 kipindi cha pili.

Katika dakika ya 71 Harry kane tena akawatungua Stoke City kabla ya Dele Ali kuhitimisha ushindi huo kwa bao la nne katika dakika ya 82.

Mshambulia Harry Kane amefikisha idadi ya mabao 24 akifuatiwa na Jamie Vardy mwenye 22 huku Sergio Aguero akiwa na mabao 21.