Timu ya Kenya ya Raga yakaribishwa kwa shangwe

Image caption Mashabiki na wachezaji wa timu ya Kenya

Biashara zote zilisimama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya huku shangwe na nderemo zikitawala eneo hilo siku ya Jumanne wakati timu ya mchezo wa raga ya Kenya ya wachezaji saba kila upande ilipowasili baada ya ushindi wake huko Singapore.

Huwezi kusikiliza tena

Ndege ya Qatar Airline iliowabeba mashujaa hao kutoka Doha ilitua mda mfupi baada ya saa nane na nusu na kuwapeleka wachezaji hao katika eneo la watu maarufu ambapo nahodha wa timu hiyo Andrew Amonde alikuwa wa kwanza kujitokeza.

Miongoni mwa wale walioilaki timu hiyo ni pamoja na waziri wa michezo Hassan Wario na Mwenyekiti wa muungano wa wachezaji wa raga Richard Omwela.

Image caption Wachezaji wa timu ya raga ya Kenya

Kenya iliicharaza Fiji 30-7 ili kuweza kushinda taji hilo.

Ni mara ya kwanza kwa Kenya kushinda taji hilo katika msururu wa mashindano ya 7s duniani baada ya kufika fainali mara mbili mjini Adelaide 2009 na Wellington 2013.