Yanga hoi,Mazembe nao watupwa nje

Wakicheza Ugenini huko Nchini Misri, Yanga wamefungwa 2-1 na Al Ahly na kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa Africa.

Mabingwa watetezi Tp Mazembe wakaondolewa katika michuano hiyo baada ya sare ya 1-1 dhidi Wydad de Casablanca, na Casablanca wakisonga mbele kwa ushindi 3-1.

Enyimba wakasonga mbele kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Etoile du Sahel ,As Vita Club nao wakasonga mbele licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 na Mamelod Sundowns .

Al Ahli Tripoli wakawachapa Asec Mimosas kwa mabao 2-1 lakini asec akisonga mbele kwa kwa jumla ya mabao 3-2.