West Ham,Liverpool, Man United zapeta

Image caption West Ham

ligi kuu England imeendelea kwa michezo mitatu kupigwa huku timu za West Ham, Liverpool,Man United wakishinda michezo yao. Wagonga nyundo wa West Ham wameibuka na ushindi wa maboa 3-1 dhidi ya Watford, mshambuliaji Andy Carrol, akifunga goli la kwanza dakika ya 11 kisha kiungo Mark Noble akifunga mabao mengine mawili kwa mikwaju ya penati.

Liverpool wakashinda dabi yao kwa kuwachapa Everton kwa mabao 4-0, mabao ya majogoo hao yakifungwa na Divock Origi,Mamadou Sakho,Daniel Sturridge,Philippe Coutinho.

Nao mashetani wekundu wa Man United wakaibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace, beki Damien Delaney alianza kuipa Man United goli la kuongoza baada ya kujifunga kisha beki wa kiitaliano Matteo Darmian akaongeza bao la pili na kuipa timu yake alama tatu muhimu.