Nadal amshinda Montanes

Haki miliki ya picha Getty

Nyota namba tano kwa ubora wa mchezo wa tetesi kwa upande wa wanaume Rafael Nadal ameshinda mchezo wake dhidi ya Albert Montanes katika michuano ya wazi ya Barcelona.

Nadal alimshinda mpinzani wake kwa seti mbili katika seti ya kwanza akishinda kwa 6-2 na ya pili akishinda kwa 6-2.

Hivyo nyota huyu atachuana na Muitaliano Fabio Fognini ambae nae alimshinda Viktor Troicki.

Fognini alimshinda Nadal katika raundi ya tatu ya michuano ya msimu uliopita hivyo Nadali atakua na kazi kubwa ya kulipa kisasi katika mchezo ujao dhidi ya muitaliano huyo.