MOJA KWA MOJA: Man City dhidi ya Stoke City

Manchester City haijamaliza nje ya timu nne bora katika ligi ya Uingereza kwa kipindi cha misimu mitano iliopita laini huenda wakashindwa kuliafikia hilo iwapo hawatakuwa makini.Na mechi imekamilika

16.17pm:Gooooooooooal Iheanaccho aifungia manchester City bao la nne hapa baada ya uvamizi uliofanywa katika lango la Stoke City

Manchester City wanafanya mabadiliko Aguerro anatoka

Image caption Iheanacho

16.06pm:Gooooooooal Iheanaccho aipatia manchester City bao la tatu hapa katika uwanja wa Etihad.

Manchester City 3-0 Stoke City

Joe Hart anaokoa shambulizi jengine la Stoke hapa kunako dakika ya 62

16.02pm:Kona kuelekezwa Stoke.Inapigwa Toure anasukuma mkwaju wa kimo cha nyoka lakini kipa wa Stoke anautia mkobani mpira.

16.01pm:Timu ya Manchester City huenda itajilaumu iwapo itaendelea kuwawacha washambuliaji wa Stoke kuvamia lnago lake

Image caption Silva anatoka Delf anaingia

15.59pm:Manchester City inafanya mabadiliko hapa na David Silva anatoka huku Fabian Delph akiingia.

15.57pm:Stoke inaendeleza mashambulizi dhidi ya Manchester City hapa kupitia mame Diouff lakini bahati haijataka

Image caption Mashambulizi ya Stoke City

15.52pm:Stoke City inaanza kwa kufanya mashambulizi makali hapa lakini bahati inakataa kusimama.

Kipindi cha pili cha mechi kinaanza hapa katika uwanja wa Etihad huku wenyeji Manchester City wakiwa wanaongoza

Image caption Mamadou Sakho wa Liverpool

Beki wa liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA kwa madai ya kukiuka ukaguzi wa dawa za kulevya

15.34pm:Na kipindi cha kwanza kinakamilika hapa ikiwa Manchester City wanaongoza kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Stoke City

15.29pm:Manchester City 2-0 Stoke City

Image caption Aguerro

15.28pm:Aguerooooooooo Goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal .aiweka kifu mbele hapa Manchester City ikiwa ni bao la pili dhidi ya Stoke City

15.20pm:Manchester City wapata penalti dhidi ya Stoke City.sergio Aguerro anapiga.

Image caption Stoke dhidi ya Man City

15.19pm:Goaaaaaaaaaaaaal Manchester Citu inajipatia bao la kwanza hapa kupitia Fernando

15.10pm:Stoke City wapata nafasi ya wazi hapa baada ya gusa niguse katika lango la man City lakini mshambuliaji Joselu apiga kichwa na mpira unatoka nje

15.05pm:Manchester City sasa inafanya mashambulizi kwa lango la Stoke lakini mabeki wa stoke wanakataa kata kata.

Image caption Stoke City dhidi ya Man City

15.00pm:Stoke City inajitahidi hapa huku man City ikijaribu kushambulia lango la Stoke

14.55pm:Safu ya mashambulizi ya Man City inaongozwa na Aguerro na Iheanaccho

14.50pm:Manchester City inaanza kwa kasi hapa huku ikijaribu kujinoa dhidi ya Stoke City katika maandalizi ya kukabiliana na Real Madrid katika mechi ya nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya wiki ijayo.

Image caption Kikosi cha Manchester City
Image caption Kikosi cha Stoke City

14.45pm:Manchester City vs Stoke City