Juventus yatwaa taji la Serie A

Haki miliki ya picha epa

Klabu ya Juventus imetwaa Ubingwa wa Serie A huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo.

Ushindi huo umekuja baada ya Timu ya Pili kwenye Ligi Napoli kufungwa 1-0 na AS Roma huko Stadio Olimpico Jijini Rome.

Juve waliifunga Fiorentina Bao 2-1 na kuhitaji Pointi 1 tu ili kujihakikishia Ubingwa lakini kipigo cha cha Napoli kimehakikisha hawawezi tena kuikamata Juve huku Mechi zikibaki 3.

Juve sasa wana Pointi 85 wakifuatiwa na Napoli wenye Pointi 73 na AS Roma wana Pointi 71.

Kwa kutwaa Ubingwa Msimu huu, Juve walionyesha umahiri mkubwa kwani hapo Oktobo 28 walikuwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara wa Serie A.

Lakini baada ya hapo, Juve walishinda Mechi 24 kati ya 25 za Ligi zilizofuatia na kutoka Sare 1.

Katika Mechi hiyo Bao la ushindi la AS Roma lilifungwa Dakika ya 89 na Radja Nainggolan kutokana na ushirikiano mwema wa Mkongwe Totti, Pjanic na Mohamed Salah.