Liverpool yachapwa Europa League

Liverpool Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liverpool walichapwa 1-0

Mechi za kwanza za nusu fainali za Uefa Europa League zimechezwa jana, mabingwa watetezi Sevilla wakicheza ugenini na Shakhtar Donetsk.

Matokeo ya mchezo huo ni kwamba Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo.

Sevilla ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 6 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Mchin Perez, na Shakhtar Donetsk kusawazisha bao hilo dakika ya 23 kupitia kwa Maros Romeo na Stepanenko kuongeza bao la pili dakika ya 35 kipindi cha kwanza.

Baadaye kelvin Gameiro akaisawazishia Shakhtar Donetsk ikasawazisha bao hilo dakika ya 82 kwa njia ya penati .

Katika mchezo mwingine Klabu ya England Liverpool ikicheza Ugenini huko Uhispania imeambulia kichapo cha bao 1-0 mikononi mwa Villarreal kwa bao la Adrian Lopez la dakika ya 90 ya mchezo.

Timu zote nne zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo, ikiwa ni mechi za pili hatua ya nusu fainali.