Barcelona: Tunakabiliwa na upinzani mkali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Luis Enrique na Lionel Messi

Klabu ya Barcelona italazimika kushinda mechi zake zote za mwisho ili kushinda taji la ligi ya La Liga kwa kuwa huenda wapinzani wao wasipoteze hata pointi moja kulingana na kocha Kuis Enrique.

Viongozi Barcelona walioanza mwezi wa April wakiwa na pointi nane kileleni mwa ligi hiyo,wako sawa kwa pointi na Atletico Madrid huku Real Madrid ilio nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa pointi moja.

''Haiwezekani kwamba timu zilizo nyuma yetu zitapoteza pointi'',alisema Enrique siku ya Ijumaa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Real Madrid na Atletico Madrid

''Mchezo wetu ni mzuri katika kipindi hiki cha mwisho''.

Barcelona iko mbele ya Atletico kutokana na tofauti ya mabao.

Barca,Atletico na Real Madrid zote zinacheza Jumamosi katika muda tofauti.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Real Madrid dhidi ya Barcelona

KIabu ya Zinedine Zidane inaweza kwa masaa machache kupanda katika kilele cha ligi iwapo itashinda dhidi ya Real Sociedad katika mechi ya mapema.