Swansea yaichapa Liverpool 3-1

Image caption Andre Ayew akifunga bao la pili dhidi ya Liverpool

Mshambulizi wa Black Stars ya Ghana Andre Ayew alifunga mabao mawili na kuisadia timu yake ya Swansea kujihakikishia nafasi katika ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.

Ayew alifunga mabao hayo Swansea City ilipojifurukuta na kuiadhibu Liverpool 3-1.

Ayew alifungua kibano hicho kwa mkwaju wa kichwa kabla ya Jack Cork kufuma kimiani mkwaju ulioipa swansea uongozi wa mabao mawili kwa nunge kufikia muda wa mapumziko.

Hata hivyo vijana wa Jurgen Klopp walirejea uwanjani kwa kishindo.

Christian Benteke alirejeshea Liverpool matumaini kwa kufunga bao mapema katika kipindi cha pili.

Lakini Ayew akawazimia nuru kabisa katik mechi hii alipofunga bao lake la tatu na la ushindi dakika mbili tu baadaye kunako dakika ya 67.

Image caption Swansea wamejihakikishia nafasi ya ligi kuu msimu ujao

Masaibu ya Liverpool yaliongezeka Brad Smith alipooneshwa kadi yake ya pili ya njano na hivyo kulazimika kuiaga mechi hiyo.

Kufuatia kichapo hicho Liverpool sasa haina budi kujinga ukanda iliangalau waweze kushinda kombe la Europa iwapo bado wanamatumaini ya kushiriki katika kombe la mabingwa barani ulaya mwakani.

Kwa upande wao Swansea, ambao wanaorodhewshwa katika nafasi ya 13 wamejizolea alama 11 zaidi ya Sunderland ambayo iko katika hatari kubwa ya kushushwa daraja msimu ujao.