Marekani yaitaka Urusi imkomeshe Assad

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani yaitaka Urusi imkomeshe Assad

Marekani inasema kuwa inashughulikia mipango fulani ili kuzuia kulipuka upya kwa mapigano nchini Syria na kufufua usitishwaji wa maovu kote nchini humo.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema kuwa ajenda kuu ni kuzuia umwagikaji wa damu mjini Allepo ambapo zaidi ya watu 200 wameuawa ndanu ya wiki moja, kufuatia mashambulizi makubwa ya angani yanafanywa na seriki na pia makombora yanayofyatuliwa na waasi.

Marekani imekuwa ikiishawishi Urusi ikiitaka iishinikize serikali ya Syria kuachana na kile inachosema kuwa mashambulizi ya kiholela .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Urusi inasisitiza kuwa mashambulizi ya mjini Allepo ni sehemu mapigano dhidi ya makundi ya kigaidi.

Hata hivyo Urusi inasisitiza kuwa mashambulizi ya mjini Allepo ni sehemu mapigano dhidi ya makundi ya kigaidi.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani John Kerry leo Jumapili atakuwa mjini Geneva kuzungumzia hali ilivyo pamoja na mjumbe maalum ya umoja wa mataifa nchini Syria Staffan de Mistura pamoja na mawaziri wa kigeni wa Jordan na Saudi Arabia.