Djokovic atwaa ubingwa Madrid

Haki miliki ya picha Reuters

Nyota wa mchezo wa tenesi Novack Djokovic ameshinda ubingwa wa michuano ya wazi ya Madrid.

Djockovic ametwaa ubingwa huo baada ya kumshinda bingwa mtetezi wa michuano hiyo mwingereza Andy Murray kwa jumla ya seti mbili.

Katika seti ya kwanza alishinda kwa 6-2 kisha akapoteza kwa 3-6 nakumaliza na ushindi wa 6-3 katika seti ya mwisho.

Kushindwa kwa Murray kutasababisha kushuka kutoka nafasi ya pili katika katika viwango vya ubora vya mchezo huu na nafasi yake kuchukuliwa na Roger Federer anayeshika nafasi ya au kwa ubora.