Je,kombe la FA litamnusuru Van Gaal?

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Kocha Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal bado anaamini kwamba kilabu yake inaweza kufuzu katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya lakini mambo sio mazuri sana kwa upande wake na hivyobasi anatarajia kushinda kombe la FA.

Iwapo United itashinda ataufanya ushindi kuwa ufanisi mkubwa kwa kilabu hiyo na atakuwa na uwezo wa kusema kuwa imejishindia taji kubwa tangu meneja wa kilabu hiyo Alex Ferguson ajiuzulu mwaka 2013.

Hatahivyo haitatosha kusema kuwa Van Gaal anaielekeza United katika upande unaohitajika licha ya kuwashirikisha vijana kupitia mchezaji Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 18 pamoja na usajili wa Antony Martial mwenye umri wa miaka 20.

Mkurugenzi mkuu wa kilabu hiyo Ed Woodward anataka kocha wake kufaulu lakini hatma yake ya siku za usoni haijulikani.