Michuano ya CAF kuhusisha timu 16 mwakani

Haki miliki ya picha caf
Image caption Michuano ya CAf kuhusisha timu 16 mwakani

Mechi za mchujo wa ligi ya mabingwa barani Afrika na ile ya Mashirikisho zitajumuisha timu 16 kuanzia mwakani ,Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza.

Timu hizo 16 zitagawanywa katika makundi 4 ya timu nne kila mmoja badala ya 8 zilizoko sasa.

Mabadiliko hayo yalitangazwa na rais wa shirikisho la soka barani Afrika Caf Issa Hayatou

Hayatou alikuwa akizungumza katika kongamano lake huko Mexico.

Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino alishiriki katika kongamano hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabadiliko hayo yalitangazwa na rais wa shirikisho la soka barani Afrika Caf Issa Hayatou

Hayatou alitumia fursa hiyo kunadi ombi la kuongezwa kwa idadi ya mataifa yanayowakilisha bara la Afrika katika mchuano wa kombe la dunia.

Kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka wa 2015 ilishirikisha Nigeria na Mali.

Kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 20 ilihusisha Senegal na Mali, kwa hivyo ninafikiri kuwa hiyo ni sababu tosha ya kuiongezea Afrika uwakilishi katika kombe la dunia alisema bwana Hayatou.