Mabondia wa Afrika kugombea mikanda Dar es salaam

Mabondia wa Tanzania pamoja na mabondia kutoka nje ya Tanzania wamepima uzito kabla ya mapambano ya masumbwi ya kimataifa yatakaofanyika Jumamosi uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mabondia wa Tanzania watakaopanda Ulingoni ni Thomas Mashali, Abdallah Pazi, Fransic Miyeyusho, Lulu Kayage na Swalehe Mkalekwa.

Wengine ni Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi, Bondia Sajjabi Ben wa Uganda, Alan Kamote .

Bondia Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' atakuwa anagombea ubingwa wa dunia mkanda wa U.B.O kilo 76 dhidi ya bondia Sajjad Mehrab kutoka Iran, Cosmas Cheka atakuwa akigombea ubingwa wa Dunia wa U.B.O uzito wa Unyoya kilo 59 dhidi ya Fransic Kimani kutoka kenya .

Mratibu wa Mapambano hayo katibu mkuu wa shirikisho la masumbwi Tanzania Anthony Ruta amethibitisha kufanyika kwa mapigano hayo.