Mikel Arteta kuondoka Arsenal

Arteta Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arteta alijiunga na Arsenal 2011

Nahodha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuhama klabu hiyo majira haya ya joto.

Arteta pamoja na kiungo wa kati mwenzake Tomas Rosicky wanatarajiwa kuondoka baada ya mikataba yao kumalizika.

Arteta, 34, alijiunga na klabu hiyo 2011 na amewachezea mechi 150 na kufunga mabao 17.

Rosicky, 35, alijiunga na Arsenal 2006 na alituzwa kwa kuwachezea Gunners mechi 246 kipindi cha miaka 10 wakati wa mechi yake ya mwisho dhidi ya Aston Villa Jumapili.

Arteta, aliyenunuliwa Everton kwa £10m, alionekana akitokwa na machozi baada ya mechi hiyo kumalizika.

Meneja Arsene Wenger amesema wachezaji hao wawili walikuwa wa kipekee.