Terry aongeza mwaka mmoja Chelsea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Terry

Beki wa Chelsea John Terry ametia saini kandarasi mpya ya mwaka mmoja na kiliabu hiyo ya Uingereza.

Katika hotuba iliojaa hisia baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Leiceter siku ya Jumapili,mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye kandarasi yake ilikuwa imekamilika alisema kuwa angependa kusalia katika klabu hiyo.

''Kila mtu anajua mimi ni shabiki wa Chelsea '',alisema beki huyo wa Uingereza.

''Nasubiri msimu ujao tukiwa na mkufunzi mpya na natumai tutafanikiwa''.

Terry ameichezea Chelsea mara 703 katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuanza kucheza soka katika kilabu hiyo mwaka 1998.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck alisema kuwa: tunafurahi kwamba John atahudumia mwaka mwengine akiwa katika klabu hii.