Rooney kuwacha safu ya mashambulizi

Image caption Wayne Rooney

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na Uingereza Wayne Rooney amesema kuwa huenda akaanza kucheza katika safu ya kati katika siku za usoni baada kucheza vyema katika safu hiyo dhidi ya Bournemouth katika uwanja wa Old Trafford.

Katika mechi hiyo ya kufunga lgi ya uingereza,man United ilipata ushindi wa maba0 3-1 .

Nahodha huyo wa kikosi cha Uingereza alifunga bao la kwanza kabla ya kumpatia pasi nzuri Ashley young kwa bao la tatu.

''Mara nyengine unafaa kuamua katika kazi yako na kwa sasa ni bora mimi kucheza katika safu ya kati'',alisema.

''Inaweza kuwa tofauti kwa timu ya Uingereza ambapo ninaweza kuwa mshambuliaji, lakini pengine msimu ujao huenda nikacheza katika safu hiyo''.