Kenya yakubaliana na mpango wa Olimpiki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanariadha wa Kenya

Serikali ya Kenya imekubalina na mpango utakaongeza uwezekano wa wanariadha wa nchi hiyo kushiriki katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio mwezi wa 8 mwaka huu.

Taasisi ya kupambana na dawa za kuongeza nguvu michezoni ilipa nchi ya Kenya adhabu ya kutoshiriki katika michuano hiyo Mei 12 baada ya kushindwa kuwasilisha ushahidi juu ya tuhuma hizo kwa wanamichezo wake. Kama Kenya watabakia katika kizuizi hicho,chama cha riadha ulimwenguni kinaweza kuwafungia wanariadha wa nchi hiyo katika michezo hiyo. Lakini serikali ya Kenya imesema ni lazima iwe na uwakilishi katika michuano ya Rio 2016. Kama nchi hiyo itakosa michuano ya Olimpiki mwaka huu itamaanisha kuwa baadhi ya wakimbiaji wake maarufu watakosa pia nafasi ya kupata tuzo mbalimbali. Miongoni mwao ni David Rudisha ambaye atakosa nafasi ya kutetea taji lake aliloshinda mwaka 2012 mjini London katika mbio za mita 800. Nchi ya Kenya iliongoza mwaka jana katika mashindano ya Riadha ya ulimwengu mjini Beijing kwa kuwa na medani saba za dhahabu.