'David Ginola anusurika kifo'

Haki miliki ya picha PA
Image caption David Ginola

Aliyekuwa winga wa timu ya Ufaransa David Ginola anaendelea kupata afueni hospilini mjini Monaco baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Mchezaji huo mwenye umri wa miaka 49 ambaye aliwahi kuichezea Newcastle,Tottenham,Aston Villa an ambaye alijiuzulu mwaka 2002 alianguka na kuzirai kusini mwa Ufaransa.

Daktari aliyemfanyia upasuaji huo amesema kuwa Ginola alinusurika kifo.

Ujumbe wa Twitter kutoka kwa nyota huyo wa zamani ulisema: Walimwengu hamjambo,sikulala vizuri.Niko salama ,ijapokuwa nataka kupumzika kiasi.

David alicheza katika mechi ya hisani .Lakini ghafla akaanguka na kuzirai huku watu wakidhani ilikuwa mzaha lakini baada ya dakika mbili wakabaini mchezaji huyo yupo hatarani,alisema Gilles Dreyfus,profesa wa upasuaji katika hospitali ya kukabiliana na magonjwa ya moyo huko Monaco.