Blackwell sasa asema Eubank Jr hana 'utu'

Image caption Eubank Jr

Bondia aliyejiuzulu Nick Blackwell amesema kuwa Chris Eubank jr na babaake hawana utu kulingana na vile walivyofuatilia jeraha lake baada ya pigano.

Blackwell mwenye umri wa miaka 25 alivuja damu katika ubongo katika pigano alilopoteza kwa Eubank Jr ,mnamo mwezi Machi na kuwekwa katika hali ya kukosa fahamu.

Eubank alifanya mkutano na wanahabari baada ya pigano hilo la uzani wa kati ,wakati Blackwell alipokuwa hospitalini.

''Familia yangu na marafiki waliwataka kutozungumza lakini walikataa'',Blackwell aliliambia gazeti la the Sun.

''Nilikuwa sina fahamu na waliendelea na kuitisha mkutano na vyombo vya habari''.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Eubank Jr na babake

''Nimeonyeshwa kanda ya mkutano huo wa vyombo vya habari na najua kilichofanyika,si utu walivyofanya''.

Blackwell aliamka wiki moja baadaye bila ya kuhitaji upasuaji.