Semenya ashinda mbio za Diamond League

Mwanariadha Caster Semenya kutoka Afrika Kusini ameshinda mbio za 800m za wanawake katika mashindano ya Diamond League yaliyofanyika Rabat, Morocco.

Hii ni mara ya kwanza kwa msururu wa mashindano hayo kuandaliwa barani Afrika.

Semenya, 25, alifanyiwa uchunguzi wa kubaini jinsia yake kamili baada yake kushinda dhahabu mashindano ya ubingwa wa riadha ya mwaka 2009.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Semenya anatarajiwa kushinda dhahabu Olimpiki

Alimaliza mbio hizo za mjini Rabat katika muda sekunde 56.64, muda bora zaidi mwaka huu.

Anapigiwa upatu kushinda dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu mjini Rio 2016, ambapo anapanga pia kukimbia mbio za 400m.

Mwingereza Lynsey Sharp alimaliza wa tano.