Man United yazungumza na Mourinho

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jose Mourinho

Wawakilishi wa Jose Mourinho watakutana na maafisa wa klabu ya Manchester United siku ya Jumanne huku raia huyo wa Ureno akijiandaa kuchukua ukufunzi wa klabu hiyo.

Ajenti wa Mourinho Jorge Mendes ,alisafiri hadi Manchester United siku ya Jumanne asubuhi na ataongoza majadiliano hayo.

Makubaliano huenda yasitangazwe siku ya Jumanne lakini thibitisha kuwa Mourinho atamrithi Louis van Gaal linatarajiwa wiki hii.

Louis van Gaal mwenye umri wa miaka 64 alifutwa kazi kama mkufunzi wa Man United siku ya Jumatatu ,siku mbili baada ya kushinda kombe la FA.

Raia huyo wa Uingereza aliweza kuiongoza United kuchukua nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza msimu huu na kushindwa kuwasaidia kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Van Gaal pia alishtumiwa kwa kushindwa kuimarisha mchezo mzuri wa mashambulizi huku United ikifunga mabao 49 pekee msimu huu.